Akiba

Akiba ni sehemu ya kipato au rasilimali inayohifadhiwa kwa matumizi ya baadaye, badala ya kutumika mara moja. Ni utaratibu wa kuweka fedha au mali kando kwa ajili ya mahitaji ya dharura, malengo ya muda mrefu kama elimu, ujenzi, au uwekezaji wa baadaye.

Umuhimu wa kuweka akiba ni mkubwa katika maisha ya kila siku. Kwa mfano, wakati wa dharura kama ugonjwa, ajali au kupoteza kazi, akiba inaweza kusaidia mtu kuendelea na maisha bila kutetereka. Vilevile, mtu anaweza kutumia akiba kutimiza ndoto au malengo ya maisha kama kusomesha watoto au kuanzisha biashara. Kwa hiyo, kuweka akiba si tu suala la kifedha, bali pia ni sehemu ya kupanga maisha kwa busara na kuwa tayari kwa hali zisizotarajiwa. Akiba inaweza kuanza kutoka TZS 50,000/= an kuendelea kwa mwezi, na kila mwanachama anaweza kuichangia moja kwa moja kwenye akaunti ya IAASACCOS LTD. Hii ni hatua ndogo leo, lakini inaweza kuwa msaada mkubwa kesho!