HUDUMA YA RAMBIRAMBI
Rambirambi ni huduma ambayo kila mwanachama huchangia Tzs. 30,000 kwa Mwaka kwenye mfuko wa
rambirambi kwa lengo la kuwahudumia Wanachama pale wanapofariki au kufiwa na wategemezi wao
kama ilivyoainishwa katika sera ya Rambirambi. Rambirambi hiyo hutolewa kama ifuatavyo:-
- Ikiwa Mwanachama ama mwenza wa Mwanachama amefariki Chama humpatia pole ya msiba kwa
kiasi cha TZS. 1,000,000/-.
- Ikiwa mwanachama amepatwa na msiba wa wazazi au watoto, chama humpatia pole ya msiba kwa
kiasi cha TZS. 500,000/-.
Masharti ya Kupata Huduma ya Rambirambi
- Mwanachama atawasilisha kwenye Chama taarifa za wategemezi wake kwa kujaza fomu.
- Mwanachama hatanufaika zaidi ya mara moja katika kila nafasi ya mtegemezi isipokuwa kwa
nafasi ya mtoto.
- Mwanachama anatakiwa kuhuisha taarifa za wategemezi wake kila mara inapotokea mabadiliko
ya wategemezi wake.
- Mwanachama hatalipwa rambirambi endapo hachangii au anadaiwa limbikizo lolote la mchango
kabla ya janga la kifo kutokea.
- Mwanachama hatanufaika zaidi ya mara moja katika kila nafasi ya mtegemezi isipokuwa kwa
nafasi ya mtoto.
- Taarifa ya kifo itawasilishwa kwa Meneja wa Chama kwa njia rasmi ya mawasiliano. Chama
kinaweza kujiridhisha kwa njia mbalimbali juu ya taarifa ya kifo iliyowasilishwa na
mwanachama, ikiwemo kuwasiliana na kuomba uthibitisho kutoka Idara ya Rasilimali Watu,
IAA.