Jinsi ya Kujiunga na IAA Saccos

Jinsi ya Kujiunga na IAA Saccos

Fuata hatua hizi kwa kujiunga na IAA Saccos na kuanza safari yako ya kifedha

Hatua za Kujiunga

1

Pakua Fomu ya Kujiunga

Pakua fomu ya kujiunga na IAA Saccos kutoka kwenye tovuti yetu au tembelea ofisi yetu kupata nakala ya fomu.

2

Jaza Fomu kwa Usahihi

Jaza fomu kwa makini na uhakikishe maelezo yote ni sahihi. Ambatanisha hati zifuatazo:

  • Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa
  • Cheti cha Ndoa (ikiwa unayo)
  • Vyeti vya watoto(ikiwa unao)
3

Wasilisha Fomu

Wasilisha fomu kwa njia mbili:

Ofisi ya IAA Saccos (Arusha Campus)

Peleka fomu moja kwa moja kwenye ofisi yetu

Barua Pepe

Tuma nakala kwa Meneja wa Saccos:

manager@iaasaccos.co.tz
4

Thibitisha Uanachama

Baada ya kupokea na kukagua fomu yako, tutakutumia uthibitisho wa uanachama na maelezo ya akaunti yako.

Mchakato wa uthibitisho unachukua siku 1-5 za kazi