Mkopo wa Maendeleo

Mkopo wa Maendeleo

Mkopo huu unatolewa kwa kiwango kisichozidi cha shilingi milioni sabini (70,000,000/-). Mwanachama ataruhusiwa kukopa tena iwapo atakuwa amemaliza mkopo wa awali, au amerejesha moja ya tatu (1/3) la deni la awali.

  • Mwanachama ana uhuru wa kukopa kiwango ambacho hakizidi mbili na nusu (2.5) ya Akiba.
  • Riba kwa mkopo wa maendeleo ni asilimia 11% (Reducing Method).
  • Muda wa juu wa marejesho ya mkopo ni miezi arobaini na nane (48).

Jinsi ya kurejesha Mkopo

Urejeshaji wa mkopo unaweza kufanyika kwa njia ya makato ya mshahara au kulipa Benki kupitia akaunti za Chama.