Akaunti ya Amana

AKAUNTI YA AMANA

Akaunti ya Amana ni akaunti ya akiba ambayo inamuwezesha mwanachama kuendelea kuchangia kwa kuwekeza katika akaunti hiyo bila kutoa fedha kwa kipindi cha kuanzia mwaka mmoja (1).


Faida za Wekeza Akaunti

  • Riba ya asilimia tano (5%) inalipwa kila mwaka kama faida kwa mwanachama anayewekeza kuanzia milioni moja (1,000,000/-).
  • Mwanachama anaweza kuchagua kulipwa riba yake au kuendelea kuiwekeza katika akaunti yake ya wekeza.
  • Mwanachama anaweza kuamua kuhuisha kipindi kipya cha uwekezaji wa mwaka mwingine kila mwisho wa mwaka.
  • Mwanachama anaweza kuchangia katika Akaunti hii kila anapopata fedha (kwa njia ya mshahara au kuweka fedha benki (Bank Deposit)).